top of page
Search

11. Vicky Lyrics

Writer's picture: Dyler RutherDyler Ruther

11. Vicky

Ukiishi na usiye mpenda utaishi kama mtumwa

Nsikize na kwambia utajuta na utaumia

Vicky

Yeah

Mzazi


Binti Vicky Mungu amekupa uzuri hakika rangi tamu shape unakusanya kila rika sifa zako hatari yako kila kona zinasikika hata mzee anajisifu kwe pale Mungu kapika

Tangu chekechea we ni moto sio wakufika vidume hawaishi wanazidi tiririka

Umeona aina zote wabunge pastor na mizuka

Wazee wenye familia magwiji wakutupia na maskini mla bamia wote kwako wamefika

Kuchagua herufi moja toka A mpaka Z sio kama kuchagua toka A mpaka C

Wangapi kati ya wale mia wanaupendo wenye nia kati ya wale wenye nia wangapi watakuvumilia kukuskiza kwenye mia mtakapo zifunga nia

Vicky dunia inamwangalia

Hasa familia

Na bado maisha pia

Vicky anaumia

Vicky Analia

Vicky

vicky


Usirukie ndoa mama fata moyo utaepuka huzuni utaepuka karaha ya moyo

Wahenga walisha sema mdogo mdogo huvuta heri hivyo tulia dada

Usirukie ndoa mama fata moyo utaepuka huzuni utaepuka karaha ya moyo

Wahenga walishasema mdogo mdogo huvuta heri hivyo tulia dada

Ona sasa yanayokupata wewe

Amekuacha sasa unalia na wana

Oooh oohhh

Ona sasa Vicky Vicky umepoteza furaha yako

Una majonzi kupindukia aaahhh


Vicky amejikaza anatafuta mapenzi ya kweli

Kamaliza chuo ila wana wote matapeli

Shirini na sita ramani hazisomeki

Simu kila day mama anaulizaga vipi

Friends everyday kadi yako hii Vicky

Njoo nsismamie naomba nichangie Vicky

Pressure juu juu sio kwamba Vicky alipi

Wahuni wanaomtaka wote kwao mke kiki

Vicky anawajua hawa wajinga hawa ridhiki

Pesa mali akili zote ila bado mziki

Shirini na nane uuu mama umelogwa au nini

Kila mtu ameshaolewa wewe bado hujaotea hee

Vicky Analia apendi kuja umia ila hi indo dunia tunampush kwenye nia

Vicky anaolewa mara mtoto wa kwanza mtoto wa pili mchepukp wa saba

Vicky anaumia kanisani siku saba

Kila weekend ikifika niko Mbezi kwa baba

Mkutano wa saba saba

Kagera nafata shaba

Vicky yuko haya baba

Utumwa utumwani nonutumwa nyumbani

Hamna raha ya chumbani

Wako saba siku saba ye wanane dah

Dada skiza dunia itakupelekesha achana nayo fata moyo Mungu awez kuacha


Usirukie ndoa mama fata moyo utaepuka huzuni utaepuka karaha ya moyo

Wahenga walisha sema mdogo mdogo huvuta heri hivyo tulia dada

Usirukie ndoa mama fata moyo utaepuka huzuni utaepuka karaha ya moyo

Wahenga walishasema mdogo mdogo huvuta heri hivyo tulia dada

Ona sasa yanayokupata wewe

Amekuacha sasa unalia na wana

Oooh oohhh

Ona sasa Vicky Vicky umepoteza furaha yako

Una majonzi kupindukia aaahhh

38 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


Post: Blog2_Post

Subscribe Form

Thanks for submitting!

+255674051741

©2019 by DYLER RUTHER. Proudly created with Wix.com

bottom of page